Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha, Mustafa Panju akizungumza na wananchi wa kata mpya ya Sinoni kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi..
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha, Justine Nyari, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kujinadi nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi katika kata mpya ya Sinoni jijini
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi akitoa maelekezo kwa wananchi namna ya kuwasikiliza wagombea ambapo aliwataka wasipige makofi wala kushangilia wakati wagombea hao wakijinadi.
Kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha, Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya CCM katika nafasi ya ubunge ametangaza kuelekeza nguvu zake kwa vijana wasio na ajira kwa kuwawezesha kujiajiri na kujipatia kipato
Aliyasema hayo leo wakatia akizungumza katika kampeni ya kuwanadi wagomea Ubunge wa Chama cha mapinduzi CCM, mkoani Arusha katika kata mpya Sinoni , uliohudhuriwa na wagombwa 12 wa nafasi ya Ubunge
Nyari alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili Taifa kwa sasa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana na kuahidi kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini atahakikisha vijana wanajiajiri wenyewe
Alisema kuwa katika kusaidia hilo vijana watapewa elimu ya ujasiriamali na baaade kujiajiri wenyewe hali itakayosaidia kukua kwa uchumi wa Taifa letu na vijana kuongeza kipato chao
Akawataka vijana kuacha kutumika kuleta vurugu na badala yake wawe wamoja katika kuhakikisha wanaweza kujiletea maendeleo na si vingine kwani wao wamekuwa wakitumika katika sehemu mbali mbali bila kupata manufaa stahiki
“Nawaomba vijana mujiandae kwa ajili ya kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwani nimejipanga kuhakikisha mnapata elimu ya ujasiriamali ilimuweze kujiletea maendeleo na kuongeza kipato chenu na pato la taifa”alisema Nyari.
Kwa upande wake Mustapher Panju anaeomba kupewa tiketi na CCM ya nafasi ya ubunge aliwataka wagombea wenza katika kinyang’anyiro cha ubunge kupitia ccm kudumisha upendo,mshikamano,na umoja miongoni mwao vitakavyosaidia kukuza amani ndani ya chama na kuondosha makundi ambayo yamekuwa yakikiangusha chama katika chaguzi zilizopita.
Alisema kuwa changamoto za jimbo la Arusha anazijiwa hivyo wakimpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM atahakikisha umoja,mshikamano na upendo vinatawala ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.
Panju alisema kuwa atakapopitishwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya ubunge atahakikisha kuwa anal eta maendeleo tarajiwa kwa wakati kwani yeye atakuwa mtumishi wa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.
Naye Emmanuel Ole Njoro ameomba kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge ambapo alisea akipewa ridhaa atahakikisha kuwa anadumisha Amani mshikamano na umoja miongoni mwa jamii huku akiandaa mipango ya kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kujifunza ujasiriamali ili waweze kujiletea maendeleo.
Alisema kuwa jografia ya jimbo la Arusha anaifahamu pamoja na changamoto zake hivyo anaowaomba wanachama wa CCM kuhakikisha wanampatia nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho
Kwa upande wake Thomas Munisi alisema kuwa tahakikisha changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo la Arusha anazipatia ufumbuzi pindi wanachama wa CCM watakapompatia ridhaa August 1
Alisema kuwa fedha za miradizinazokusanywa na halmashauri hazitachakachuliwa na zinaelekezwa katika miradi husika ilikuweza kulibadili jimbo la Arusha kwani nia na uwezo wa kuwatumikia wakazi wa jiji la Arusha anao hivyo ni wajibu kwa wagombea kuhakikisha wanakuwa wamoja,na mshikamano miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment