Saturday, 4 July 2015

Wabunge wengine 35 nao wamepigwa stop kuingia Bungeni kwa siku tano kuanzia leo July 4 2015



Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele…Spika akamuomba Wenje atoke nje. Wabunge wote wa UKAWA wakasema tutoe wote, Spika akasema simameni niwatoe wote, Wote wakasimama na Spika akasema endeleeni kusima, kamjui kanuni! endeleeni kusimama tu.

Akawaandika majina. Spika akataja Orodha ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwasiku tano kila mmoja kwa kosa la kumdharau Spika na kwa Mjibu wa Sheria, Spika anao Uwezo wa Kumtoa Mbunge yoyote anaye vunja kanuni za bunge.


Spika kasema, kwa mjibu wa Kanuni ya 74 moja, Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya spika na kisha kupeleka jina hilo kwenya kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge. Wabunge ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwa siku tano kila mmoja ni kwa kosa la kudharau.
1.Ezekiel Wenje

2.Mussa Kombo

3.Masoud Abdallah Salim

4.Rebecca Ngodo

5.Sabrina Sungura

6.Khatib Said Haji

7.Dr. Anthony Mbassa

8.Maulidah Anna Valerian Komu

9.Kulikoyela Kahigi

10.Cecilia Pareso

11.Joyce Mukya

12.Mariam Msabaha

13.Grace Kiwelu

14.Israel Natse

15.Mustapha Akonaay

16.Konchesta Rwamlaza

17.Suleiman Bungura

18.Rashid Ali Abdallah

19.Ali Hamad

20.Riziki Juma

21.Rukia Kassim Ahmed

22.Azza Hamad

23.Khatibu Said Haji

24.Kombo Khamis Kombo

25.Ali Khamis Seif

26.Haroub Mohammed Shamisi

27.Kuruthum Jumanne

28.Mchuchuli

29.Amina Mwidau

30.Mkiwa Kimwanga

31.Salum Baruhani

32.Marry Stellah Malaki

33Rashid Ally Omary

34.Mwanamrisho Abama

35Lucy Owenya

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge kasema anakubaliana na maamuzi ya Spika na akaomba,

Silinde asihudhulie vikao vyote vilivyo salia kwa sababu alipoitwa kujitetea kwa mjibu wa Sheria alidharau

Selasini na Halifa wapewe onyo kwani walijutia makosa waliyo yafanya na kusema hawakufanya sahihi

No comments: