Tuesday, 30 June 2015

MSAFARA WA LOWASSA WASIMAMISHWA DUMILA MKOANI MOROGORO WAKATI AKIELEKEA MKOANI DODOMA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa umati wa watu wakazi wa Mji wa Dumila, Mkoani Morogoro, waliomsimamisha ili awasalimie wakati alipokuwa safarini kuelekea Mkoano Dodoma, leo Juni 30, 2015. Mh. Lowassa anatarajia kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania, kesho Julai 1, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia...

Wednesday, 24 June 2015

LOWASSA APATA UDHAMINI WA KISHINDO JIJINI ARUSHA LEO, WANACCM 120,335 WAMDHAMINI

Add caption

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) sambamba na Mkewe Mama Regina Lowassa, wakiongozana na viongizi mbali mbali wa Chama wa Mkoa wa Arusha waliofika kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA, wakati akitokea Mkoani Dodoma kuhudhulia vikao cha Bunge na kupigia kura bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016.










Monday, 22 June 2015

ZITTO KABWE, KUITEKA MPANDA NA KUVUNA MA ELFU YA WATU


 
 

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwahutubi wakazi wa mji wa Mpanda mkoani Katavi jana, ambapo chama hicho kinaendelea na ziara za kutambulisha viongozi wake.
Mwanaharakati na Mshauri wa chama cha ACT Wazalendo, Mama Terry, akiwahutubia wakazi wa mji wa Mpanda mkoani Katavi jana, ambapo chama hicho kinaendelea  na ziara ya kutambulisha viongozi wake.


 







Sunday, 21 June 2015

Lowasa kuiteka Iringa



Mh. Edward Lowassa, akitoa hotuba ya shukrani kwa maelfu ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa mpira wa Samora jana. Mh. Lowassa alipata wadhamini zaidi ya 58,000 mkoani Iringa wakati Njombe alivuna wadhamini zaidi ya 20,000.

Saturday, 20 June 2015

Mustafa Panju kuingia katika mbio za ubunge Arusha mjini



Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha, Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia  Chama cha Mapinduzi CCM.


Lowasa kuiteka Mbeya

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa apata mapokezi mazito yaliyovunja rekodi ya mikoa yote aliyotembelea akiwa katika ziara ya kutafuta wadhamini ka ajili ya kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia CCM. Licha ya kupata mapokezi makubwa, Lowassa aliyetua katika uwanja wa Songwe jijini Mbeya hapo jana na kulazimika kusimama katika miji ya Mbalizi na Soko Matola amepata wadhamini zaidi ya 53,000.



Friday, 19 June 2015

Mkurugezi wa Bushbuck Safaris ltd Kutangaza Nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini Jana Ofisini kwake Kupitia Chama Cha CCM Kama kitampa Nafasi




 
Asalam aleykum na Bwana Yesu Asifiwe.

1.0. Awali ya yote ninaomba kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kukutana nanyi siku hii ya leo. Napenda pia kuwashukuru kwa moyo mmoja kwa kuitikia wito wangu wa kuja kwenye mkutano huu muhimu kwetu sote.

2.0. Ndugu zangu; mwaka huu wa 2015 ni mwaka muhimu kwetu sote Wa-Tanzania kwa sababu kwa mara ingine tena tunapata nafasi pekee ya kuchagua viongozi wetu watakaotuongoza katika kipindi cha miaka 5 katika ngazi mbali-mbali. Uchaguzi mkuu ulioko mbele yetu utahusu kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Wabunge,wawakilishi,masheha na Madiwani.

3.0. Ndugu Wanahabari; Kupitia kwenu mkutano wetu wa leo ni kwa ajili ya KUWATANGAZIA RASMI kwamba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu nitagombea nafasi ya UBUNGE JIMBO LA ARUSHA KUPITIA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI. Iwapo wana CCM na Chama changu kita ridhia.Nia hii nimeshawarifu Viongozi wa Chama cha Mapinduzi – Wilaya ya Arusha. Leo hii sasa ninasema rasmi kwa WAKAZI NA WANANCHI WA WILAYA YA ARUSHA kwamba wakati ukifika nitaenda ofisi ya CCM – Wilaya na kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya UBUNGE KWA MWAKA 2015.

4.0. Mimi kwa jina naitwa MUSTAFA ABDULLA PANJU ni mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi kwa kadi namba 1608369. Mimi pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utalii ya BUSHBUCK SAFARIS.

5.0. Kwa nafasi hii ya leo sitapenda kueleza matarajio yangu na ya Chama kwa Wananchi Wa Wilaya ya Arusha kwa sababu Chama bado hakijatoa ILANI YAKE YA UCHAGUZI 2015. Itakapotolewa nitaweza kueleza niliyonayo kwa maendeleo yetu ya Wilaya ya Arusha.

6.0. Kwa sasa naomba tu niseme yafuatayo muhimu sana:-
a) Ninaomba kuwashauri Wananchi na Wagombea Wenzangu kwamba KUGOMBEA SIYO KUGOMBANA. Maana imezoeleka sana na ni hatari kwamba Wagombea mara nyingi hujizolea sifa au umaarufu kwa kuwapaka upande mwingine matope, kashfa na sifa mbaya ambazo baada ya uchaguzi hugundulika siyo za kweli. Wakati huo kiongozi asiyefaa huwa ameshachaguliwa na hatasaidia Wananchi kwa kipindi cha miaka 5. Kiongozi mzuri anaachwa pembeni.
b) Kwa hivyo Wagombea wote wa nafasi ya Ubunge katika Chama lazima kujenga UNDUGU,UPENDO na URAFIKI wakati wote ili kuepuka kujenga makundi ndani ya Chama kwa misingi mbali-mbali ya UKABILA, UDINI na hata RANGI. Sisi sote ni WATANZANIA wenye nia ya kuwatumikia Wananchi kwa maendeleo ya Wilaya,Mkoa na Taifa kwa ujumla.
c) Mimi binafsi – MUSTAFA ABDULLA PANJU katika harakati hizi zinazokuja za kampeni na Uchaguzi ndani ya Chama na hata baadaye na Wenzetu wa Vyama Vingine vya Siasa sitamsema mtu binafsi au watu kwa mambo yao. ILA NITAZUNGUMZA MTAZAMO WANGU KWA MISINGI YA KIONGOZI TUNAYEMTAKA KWA KUWAONGOZA WANANCHI KWA MAENDELEO YETU WOTE.
ILANI YETU YA CHAMA 2015 ITAKUWA DIRA KATIKA KAMPENI YANGU.

7.0 Suala hili la makundi na vikundi iwe katika Chama la kwa Wananchi wote kwa ujumla tuliangalie kwa umakini ni kuliacha kabisa kwa sababu linajenga UHASAMA ndani ya Chama na pia uhasama unaoleta ubaguzi ndani ya nchi kwa ujumla. Tuombe Mwenyezi Mungu tuwe na uchaguzi wa AMANI NA UPENDO ndani ya Chama na pia wakati wa Uchaguzi Mkuu.

8.0 Ndugu zangu kwa nafasi hii naomba kurudia tena kutangaza nia yangu kwamba itakapofika wakati nitaenda kuchukua fomu kwenye ofisi yetu ya Chama Cha Mapinduzi – Wilaya.

Kwa nafasi hii nataka nitoe wito kwa Wananchi wa Arusha na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi. Ili tuweze kushinda kila mmoja aende akajiandikishe kwenye vituo vilivyoainishwa hapa wilayani.

Wakati ndio huu.

9.0 Baada ya hapo nitatekeleza yatakayofuatia kwa kuzingatia KANUNI NA SHERIA ZILIZOWEKWA NA CHAMA CHETU – KATIKA KUENDESHA KAMPENI.

10. Naomba tena kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa kuja kunisikiliza.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU TUBARIKI WATANZANIA WOTE

Ahsante Sana
Mustafa Abdulla Panju