Mbunge wa Arumeru Mashariki, Kamanda Joshua Nassari amepata
ajali ya Chopa! Kijiji cha Leguruki wilaya ya Meru mkoani arusha akiwa katika
mikutano ya kuhamasisha uandikisha.
Tunamshukuru Mungu taarifa za awali zimedai hajaumia sana
ilihali mmoja wa abiria bado jina lake halijatajwa ameripotiwa kuvunjika mguu.
Taarifa kutoka kwa Ndote Katibu wa Mbunge Mbowe juu ya
chanzo cha ajali Hii hapa
"Chopper imepigwa na storm kwa takriban dk 2. Pilot
amefanikiwa kufanya landing manouvre lakini kimbungaa kilikuwa kikali sana.
Ndege imecrash abiria wameumia kiasi tu. Wamepelekwa Selian Hospital.Ndege
imebaki vipande. Nimeongea na pilot akiwa na tune nzuri tu. Wenzake walikuwa wametangulia
hospitalini. Tuwaombee wapate nafuu haraka."