Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini
Arusha, Mustafa Panju akizungumza na wananchi wa kata mpya ya Sinoni
kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha
Mapinduzi..
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa
madini jijini Arusha, Justine Nyari, akizungumza katika mkutano wa
hadhara wa kujinadi nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi katika
kata mpya ya Sinoni jijini
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi
wa uchaguzi akitoa maelekezo kwa wananchi namna ya kuwasikiliza
wagombea ambapo aliwataka wasipige makofi wala kushangilia wakati
wagombea hao wakijinadi.
Kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa
madini jijini Arusha, Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya CCM katika
nafasi ya ubunge ametangaza kuelekeza nguvu zake kwa vijana wasio na
ajira kwa kuwawezesha kujiajiri na kujipatia kipato
Aliyasema hayo leo wakatia akizungumza katika kampeni ya kuwanadi
wagomea Ubunge wa Chama cha mapinduzi CCM, mkoani Arusha katika kata
mpya Sinoni , uliohudhuriwa na wagombwa 12 wa nafasi ya Ubunge
Nyari alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili Taifa kwa sasa ni
pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana na kuahidi kuwa endapo
atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini atahakikisha vijana
wanajiajiri wenyewe
Alisema kuwa katika kusaidia hilo vijana watapewa elimu ya
ujasiriamali na baaade kujiajiri wenyewe hali itakayosaidia kukua kwa
uchumi wa Taifa letu na vijana kuongeza kipato chao
Akawataka vijana kuacha kutumika kuleta vurugu na badala yake wawe
wamoja katika kuhakikisha wanaweza kujiletea maendeleo na si vingine
kwani wao wamekuwa wakitumika katika sehemu mbali mbali bila kupata
manufaa stahiki
“Nawaomba vijana mujiandae kwa ajili ya kupunguza wimbi la ukosefu wa
ajira kwani nimejipanga kuhakikisha mnapata elimu ya ujasiriamali
ilimuweze kujiletea maendeleo na kuongeza kipato chenu na pato la
taifa”alisema Nyari.
Kwa upande wake Mustapher Panju anaeomba kupewa tiketi na CCM ya
nafasi ya ubunge aliwataka wagombea wenza katika kinyang’anyiro cha
ubunge kupitia ccm kudumisha upendo,mshikamano,na umoja miongoni mwao
vitakavyosaidia kukuza amani ndani ya chama na kuondosha makundi ambayo
yamekuwa yakikiangusha chama katika chaguzi zilizopita.
Alisema kuwa changamoto za jimbo la Arusha anazijiwa hivyo wakimpa
ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM atahakikisha umoja,mshikamano na
upendo vinatawala ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.
Panju alisema kuwa atakapopitishwa na CCM kupeperusha bendera ya
chama hicho kwa nafasi ya ubunge atahakikisha kuwa anal eta maendeleo
tarajiwa kwa wakati kwani yeye atakuwa mtumishi wa wananchi wote bila
kujali itikadi za vyama.
Naye Emmanuel Ole Njoro ameomba kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi
ya Ubunge ambapo alisea akipewa ridhaa atahakikisha kuwa anadumisha
Amani mshikamano na umoja miongoni mwa jamii huku akiandaa mipango ya
kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kujifunza ujasiriamali ili waweze
kujiletea maendeleo.
Alisema kuwa jografia ya jimbo la Arusha anaifahamu pamoja na
changamoto zake hivyo anaowaomba wanachama wa CCM kuhakikisha wanampatia
nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho
Kwa upande wake Thomas Munisi alisema kuwa tahakikisha changamoto
zinazowakabili wakazi wa jimbo la Arusha anazipatia ufumbuzi pindi
wanachama wa CCM watakapompatia ridhaa August 1
Alisema kuwa fedha za miradizinazokusanywa na halmashauri
hazitachakachuliwa na zinaelekezwa katika miradi husika ilikuweza
kulibadili jimbo la Arusha kwani nia na uwezo wa kuwatumikia wakazi wa
jiji la Arusha anao hivyo ni wajibu kwa wagombea kuhakikisha wanakuwa
wamoja,na mshikamano miongoni mwao.