Monday, 20 July 2015

MUSTAFA PANJU AJINADI KWA WANANCHI WA JIMBO LA ARUSHA ASEMA

kasemaje-com-mustafa-panju-ajinadi-kwa-wananchi-wa-jimbo-la-arusha-asema-akipata-ubunge-hawatajutia-kamwe_f864cb83f3c443f1901a711b8618e163fc5dde86.jpg
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akiongea katika mkutano wa hadhara katika kata mpya ya Olmoti jana ambapo wagombea 12 walipata fursa ya kujitambulisha kwa wananchi na kunadi sera zao, Mustapha panju amesema kuwa kilicho msukuma kugombea nafasi hiyo ni kuakikisha wananchi wa jimbo la arusha wanapata ridhaa ya kuwa na maendeleo ya hali ya juu ikiwemo kuweza kukua kisayansi na kuweza  kufika


kasemaje-com-mustafa-panju-ajinadi-kwa-wananchi-wa-jimbo-la-arusha-asema-akipata-ubunge-hawatajutia-kamwe_58380ff2358ce92ecd8e9fb3b55667695d89b265.jpg
Mustafa Panju akiwa na wagombea wenzake wa chama hicho jana katika kata mpya ya Olmoti jijini Arusha walipokwenda kujitambulisha kwa wananchi na kunadi sera zao pia walipata fursa ya kutembelea kata ya Olasiti,Osunyai JR
kasemaje-com-mustafa-panju-ajinadi-kwa-wananchi-wa-jimbo-la-arusha-asema-akipata-ubunge-hawatajutia-kamwe_1186e675765e309d472530842c557b83cba348e3.jpg
Mtoto aliyefika kusikiliza sera za wagombea Ubunge wa chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa ameshikilia kipeperushi cha mgombea Ubunge jimbo la Arusha Mustafa Panju katika kata ya Osunyai JR
kasemaje-com-mustafa-panju-ajinadi-kwa-wananchi-wa-jimbo-la-arusha-asema-akipata-ubunge-hawatajutia-kamwe_08ce058c554a0e295ca2e15dbb02603f711f4107.jpg
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano akizungumza katika kata mpya ya Olmoti jana ambapo alisisitiza wananchi kusikiliza sera za wagombea huku akiwataka kutokupiga makofi au kushangilia wakati wakijieleza 

Sunday, 19 July 2015

DIAMOND PLATNUMZ ANG'ARA KWENYE TUZO ZA MAMA


 
Diamond Platinumz akifanya yake katika red Carpet.  DIAMOND PLATNUMZ ameibuka mshindi wa Best Live na kuwamwaga Mi Casa -South Africa, Flavour- Nigeria, Big Nuz, South Africa,Toofan-…

Friday, 17 July 2015

Mkurugenzi Wa BushBuck Safaris wakati akirudisha FORM Ya kuwania Ubunge Wa Arusha Mjini

NDUGU WANANCHI NA VIONGOZI KWANZA NAWASHUKURU KWA PONGEZI NA MAOMBI YENU KWA MWENYEZI MUNGU KWA KUNITAKIA KHERI NA USHINDI.
MUNGU AWAPE NGUVU ZAIDI NA UPENDO NA MZIDI KUSAMBAZA SALAMU KWA WANANCHI WENGINE ILI TUWEZE KWA PAMOJA KUPATA USINDI MKUBWA KWA CCM.
NINAWAARIFU KWAMBA NIMERUDISHA FOMU ZILIZO JAZWA KAMILI LEO TAREHE 17/07/2015 SAA KUMI JIONI
ASANTENI NA MUNGU AZIDI KUTUONGOZA TUPENDANE WATANZANIA.
MABADILIKO INAWEZEKANA ARUSHA
UMOJA NI USINDI



Mkurugenzi wa BushBuck Safaris Ltd Kuchukua form kugombea Ubunge wa Arusha Mjini






Ni baadhi ya waandishi wa kimuoji na kutoa neno la shukrani



NDUGU WANANCHI NA VIONGOZI WA ARUSHA. MIMI MUSTAFA PANJU (BUSHBUCK) NINAYO HESHIMA NA FURAHA KUWAARIFU KWAMBA NIMECHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM LEO TAREHE 17/07/2015
MABADILIKO INAWEZEKANA ARUSHA
UMOJA NI USHINDI





Thursday, 16 July 2015

5 wajitokeza ubunge Arusha Mjini



KINYANG'ANYIRO cha kuwania Ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini jana kilianza kwa mbwembwe baada ya wanachama watano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza kuwania ubunge katika Jimbo hilo.
Wanasheria wawili wa kujitegemea wa Jijini Arusha, Edmund Ngemela na Victor Njau ndio waliofungua pazia la kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kwa wana CCM wa Arusha Mjini kutaka kuteuliwa kuwania kiti hicho.
Njau ndiye mwana CCM aliyekwenda kuchukua fomu akiwa na msururu wa wapambe wa chama hicho, huku wakiimba nyimbo nyingi za kuwataka wanachama wa CCM kumuunga mkono mgombea huyo, ambaye wanadai ana sifa zote za kulikomboa jimbo hilo ambalo liko Chadema.
Wengine waliochukua fomu lakini hawakuwa na shangwe na mbwembwe nyingi ni Mahamudu Omari, Mosses Mwizarubi na Swalehe Kiluvia, ambao waliingia kuchukua fomu kimya kimya na kuondoka.

Wednesday, 15 July 2015

MKURUGENZI WA KIWANDA CHA MONABAN CHA JIJINI ARUSHA KUWA KAMANDA WA VIJANA UVCCM MKOA


Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw. Philemon Mollel akiwa ameshililia ngao na mkuki ikiwa ni ishara ya kusimikwa rasmi kuwa kamanda wa vijana UVCCM Mkoa katika sherehe zilizofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho. Bw. Philemon Mollel akivishwa taji.…

Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel akiapa kuwa kamanda wa vijana UVCCM Mkoa.
 
Mboni Mhita akiongea katika sherehe hizo za kusimikwa rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw. Philemon Mollel kuwa kamanda wa vijana Mkoa.

Friday, 10 July 2015

LOWASA:Napenda kumpongeza Rais Jakaya Kikwete



Napenda kumpongeza Rais Jakaya Kikwete na serikali yake kwa mafanikio makubwa katika kipindi chake cha uongozi. Binafsi pia namshukuru Rais Kikwete kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwa mtendaji mkuu wa serikali yake kwa kipindi cha miaka miwili. Serikali hii ya awamu ya nne imefanikiwa kufanya mambo mengi makubwa ya kujivunia na kwa hakika ni matarajio ya watanzania kwamba serikali ijayo itaendeleza mafanikio na juhudi za Rais Kikwete katika kumaliza tatizo la umaskini kwa watanzania.